Kilatini
| Kilatini Lingua Latina (la) |
|
|---|---|
| Lugha | |
| Asili | Italia (Dola la Roma) |
| Wasemaji |
L1 : Hakuna wasemaji wa asili |
| Familia za lugha | Kihindi-Kiulaya Kilatini-Kihispania Kilatini-Faliski |
| Aina za Awali | Kihindi-Kiulaya cha Kale Kilatini cha Kale Kilatini cha Kawaida |
| Mfumo wa kuandika | Alfabeti ya Kilatini |
| Lugha Rasmi | |
| Lugha rasmi kwa | Mji wa Vatikani |
| Nambari za Msimbo | |
| ISO 639-1 | la |
| ISO 639-2 | lat |
| Glottolog | lati1261 |

Kilatini (Lingua Latina la) ni lugha ya kale ya Kihindi-Kiulaya ambayo ilizungumzwa katika Dola la Roma. Ilianza kama lugha ya eneo la Lazio nchini Italia na baadaye ikawa lugha kuu ya utawala wa Kirumi, ikienea kote Ulaya kupitia upanuzi wa Dola la Roma. Ingawa haizungumzwi tena kama lugha ya asili, Kilatini bado hutumika katika taasisi za kidini, sayansi, sheria, na elimu ya juu, hasa katika Mji wa Vatikani na taasisi za kitaaluma. Lugha za Kirumi kama Kihispania, Kifaransa, Kiitaliano, Kireno, na Kiromania zilichipuka kutoka Kilatini cha Kawaida (Vulgar Latin), ambacho kilitumiwa na watu wa kawaida katika Milki ya Roma
Historia
[hariri | hariri chanzo]
Kilatini kilikuwa lugha hai takriban kati ya miaka 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake mbalimbali ziliendelea na kukomaa kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi, kama Kiitalia, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania n.k.
Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa Wikipedia.
Kilikuwa
- lugha ya Dola la Roma (angalia pia Roma ya Kale)
- lugha mama ya lahaja zilizoendelea na kuwa lugha za Kirumi
- lugha ya elimu na sayansi katika Ulaya kwa karne nyingi
- lugha rasmi ya serikali katika nchi nyingi za Ulaya kati ya mwisho wa Dola la Roma mwaka 476 BK hadi mnamo 1700 BK
- lugha pekee ya liturgia katika Kanisa la Kilatini hadi mwaka 1965
Hadi leo Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya. Tena ni
- lugha ya kidini katika Kanisa Katoliki
- lugha rasmi katika nchi ya Vatikano.