Ahazia wa Israeli
Mandhari

Ahazia wa Israeli (kwa Kiebrania אֲחַזְיָה, ʾĂḥazyā; 870 KK hivi - 852 KK hivi) alikuwa mwana wa mfalme Ahabu na malkia Yezebeli akatawala kwa miaka 2 Ufalme wa Israeli. Kwa kuwa hakuacha watoto, alirithiwa na mdogo wake, Yoramu.
Biblia inamhukumu hasa kwa kuendeleza sera ya kidini iliyoanzishwa na Yeroboamu I ikiwataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi, na zaidi kwa kufuat sera ya wazazi wake ya kutaka Waisraeli waabudu Baali badala ya YHWH.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Kwanza cha Wafalme, 22:51-53.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ahazia wa Israeli kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |