Lockheed AC-130
| Lockheed AC-130 | |
|---|---|
Ndege ya mapigano ya AC-130J Ghostrider kutoka Kikosi cha 4 cha Operesheni Maalum | |
| Taarifa za jumla | |
| Aina: | Ndege ya mapigano ya angani na usaidizi wa karibu wa ardhi |
| Nchi ya asili: | Marekani |
| Mtengenezaji: | Lockheed Martin Boeing |
| Safari ya kwanza: | AC-130A: 1967 |
| Ilianza kutumika: | |
| Ilipoondolewa: | |
| Hali ya sasa: | Inatumika (AC-130J) |
| Mtumiaji mkuu: | United States Air Force |
| Iliyotokana na: | |
| Aina nyingine / Matoleo | |
| AC-130A • AC-130H Spectre AC-130U Spooky • AC-130W Stinger II AC-130J Ghostrider | |
Lockheed AC-130 ni ndege ya mapigano yenye silaha nzito za kushambulia ardhini. Inatokana na ndege ya usafirishaji ya C-130 Hercules. Ndege hii inabeba safu pana ya silaha zilizounganishwa na vihisi vya kielektroniki, mifumo ya urubani, na mifumo ya kudhibiti shabaha na moto. Kwa sababu ya ukubwa wake na urefu mdogo wa kuruka wa takriban futi 7,000 (mita 2,100), operesheni zake za kutoa usaidizi wa karibu wa anga mara nyingi hufanywa usiku.
Jumba la ndege hii unatengenezwa na Lockheed Martin, wakati kampuni ya Boeing inahusika na kuibadilisha kuwa ndege ya mapigano na kuipa huduma za usaidizi.[5] Mtumiaji wake pekee amekuwa Jeshi la Anga la Marekani (United States Air Force), ambalo kwa sasa linatumia toleo la AC-130J Ghostrider. Ilitengenezwa wakati wa Vita ya Vietnam chini ya mradi wa "Project Gunship II" ili kuchukua nafasi ya Douglas AC-47 Spooky. Tangu wakati huo, imeshiriki katika mapigano huko Grenada, Panama, Vita ya Ghuba, Somalia, Bosnia, Kosovo, Afghanistan, Iraq na Libya.[6]

Ndege hii ina chumba cha marubani kisichobanwa na hewa (unpressurized cabin), na silaha zake zote zimeunganishwa ili kupiga risasi kupitia upande wa kushoto wa mwili wa ndege. Wakati wa shambulio, ndege hufanya mzunguko mkubwa angani ukizingira lengo (pylon turn), hali inayoiwezesha kuendelea kumimina risasi kwenye eneo moja kwa muda mrefu kuliko shambulio la kawaida la ndege za vita.

Katika miaka ya hivi karibuni, mfumo wa silaha wa AC-130 umeboreshwa kwa kiasi kikubwa kwa kuongezwa mizinga ya kisasa ya mm 30 na mm 105, pamoja na uwezo wa kurusha makombora yanayoelekezwa kwa usahihi wa hali ya juu kama vile AGM-114 Hellfire na mabomu ya GBU-39 au GBU-69/B Small Glide Munition.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 Slack, Chip (26 Mei 2015). "Air Commandos retire final AC-130H Spectre gunship". Cannon AFB. 27th Special Operations Wing Public Affairs. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Juni 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "AC-130U Fact Sheet". Air Force. Iliwekwa mnamo 1 Novemba 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "AC-130W Stinger II". AF.mil. Machi 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Agosti 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "AC-130J Ghostrider". Air Force. United States Air Force. Januari 2025. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Novemba 2024. Iliwekwa mnamo 2025-07-06.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ AC-130U Gunship page Archived 10 Agosti 2014 at the Wayback Machine. Boeing.
- ↑ "AC-130H/U Gunship". US Air Force. 30 Julai 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Juni 2009.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- AC-130J Ghostrider kwenye tovuti rasmi ya U.S. Air Force
- Lockheed AC-130A Hercules kwenye National Museum of the USAF
| Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |