Sukumawiki
| Sukumawiki (Brassica oleracea) | ||||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mimea ya sukumawiki shambani | ||||||||||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Sukuma wiki ni mboga ya majani maarufu sana ukanda africa mashariki amabayo yanatokana na mmea wake ujulikana kwa jina la sukuma wiki majani yake yanakatwa katwa na kuchanganywa na viungo vingine kama karoti, vitunguu, nyanya na viungo mbalimbali. chakula hiki hupendwa sana na huliwa mara kwa mara pamoja na ugali uliotokana na kusaga mahindi na kupata unga.[1] [2]
nchini Tanzania, Kenya, Uganda na nchi nyingine za afrika mashariki mboga hizi za majani zinajulikana kwa jina la sukuma na wakati mwingine ufananishwa na mimea ya kale. jina lenyewe la "sukuma wiki" linamaanisha kusukuma wiki au kuyavuta maisha ili yawatoshe wiki nzima . kwani mboga hii ni ya bei nafuu na hupatikana kwa urahisi mwaka mzima katika ukanda huu. mboga hii huunda mlo mkuu pamoja na ugali wa mahindi.
Mfano wa upishi
[hariri | hariri chanzo]Katakata majani. Chemsha vikombe viwili vya maji katika sufuria. Ongeza majani yaliyokatwa katika maji. Ongeza chumvi na viungo vingine kama maji ya limau, nyanya na kitunguu kilichokatwa.
Unaweza kuingiza pia vipande vya nyama, samaki na karanga.
Picha
[hariri | hariri chanzo]- Sukumawiki ya mawimbi
- Maua
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Sukuma Wiki Recipe on "allthingskenyan"
- Sukuma na nyama Ilihifadhiwa 26 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.
- Sukuma wiki: Kenyan-style sauteed greens Ilihifadhiwa 19 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.
- Sukuma wiki recipe
- Ugali and Sukuma Wiki (East African Power Lunch) Ilihifadhiwa 8 Agosti 2011 kwenye Wayback Machine.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hobbs, Jane-Anne (2017-07-12), "15 of Africa's favorite dishes | CNN", CNN (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2026-07-25
- ↑ "The Vibrant Sautéed Greens I Cook on Repeat Every Week", Serious Eats (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2026-07-25